Harambee Stars yapata mkufunzi mpya

November 18, 2017

Shirikisho la soka nchini FKF limemteau Mbelgiji Paul Put kama mkufunzi mpya wa timu ya Taifa, Harambee stars.


Put alipewa jukumu hilo rasmi na rais wa shirikisho hilo Nick Mwandwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa FKF uliofanyika mjini Mombasa.

Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 61 amesaini mkataba wa miaka miwili ili kuchukua jukumu hilo ambalo ni lake la tatu kama mkufunzi wa timu ya taifa. Katika ukufunzi wake amewahi kuwa mkufunzi wa Gambia, Jordan na Burkina Faso.

Kibarua chake cha kwanza kitakuwa kuiongoza Harambee Stars katika mchuano wa CECAFA senior challenge cup utakaofanyika Disemba 3 huku mechi ya kwanza ikiwa ni dhidi ya Amavumbi ya Rwanda.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.