Harambee stars yatinga fainali

December 15, 2017

Wenyeji Kenya wamefuzu kwa michuano ya ubingwa wa kanda ya Afrika mashariki na kati, maarufu kama Cecafa Senior Challenge.

Kenya wamefuzu baada ya kufunga bao muda wa ziada dhidi ya Burundi katika nusu fainali iliyochezewa mjini Kisumu, Magharibi mwa Kenya Alhamisi.

Baada ya kumaliza dakika 90 bila bao, kiungo wa kati Whyvonne Isuza alifunga bao la ushindi kipindi cha kwanza muda wa kuongezwa.

Kenya, chini ya mkufunzi wao mpya Paul Put, sasa watacheza na mshindi wa nusufainali kati ya Uganda na Zanzibar kwenye fainali Jumapili.

Ushindi huo wa Kenya umeendeleza mwanzo mzuri kwa Mbelgiji Put ambaye alichukua usukani kama mkufunzi mkuu mwezi jana.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.