Harambee stars yazidi kupongezwa

December 19, 2017

Mwenyekiti wa tawi dogo la FKF Kaunti ya Mombasa Juma Goshi ameipongeza timu ya taifa ya mpira wa mguu Harambee stars kwa kunyakua ushindi wa Cecafa Senior Challenge Cup.

Akizungumza na meza yetu ya michezo kwa njia ya simu, Goshi ameipongeza afisi kuu ya FKF nchini kwa kuandaa mikakati mizuri iliyowezesha timu hiyo kunyakua ushindi.

Goshi aidha amesema kuwa Harambee Stars imeleta fahari kubwa kwa nchi ya Kenya ikizingatiwa kuwa ilikuwa imeanza kupoteza makali katika mechi za awali.

Harambee stars ilichukua ubingwa huo kwa mara ya saba kwa kuishinda Zanzibar kwa njia ya penalti Jumapili iliyopita katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.