HOTELI ZA VOI ZA HIMILI MAWIMBI YA SIASA

December 4, 2017

Baadhi ya wamiliki wa hoteli za kifahari katika kaunti ya Taita Taveta wanadai joto la kisiasa lililoshuhudiwa nchini tangu mwezi Agosti, halikuathiria biashara zao.

Kulingana na mkurugenzi wa hoteli ya LION HILL LODGE, inayopatikana mjini Voi, Agam Basil,watalii wa nje na ndani ya nchi wamekua wakitembelea kaunti hiyo kama kawaida, huku wakitarajia idadi hiyo kuongezeka zaidi msimu huu wa siku kuu ya Krismasi na mwaka mpya

Basil amesema kuwa asilimia 80 ya watalii wanaozuru kaunti hiyo wanatoka mataifa ya nje huku wa humu nchini wakiwasilisha asilimia 20.

Mmiliki huyo wa hoteli ametoa mwito kwa serikali kupitia wizara ya utalii kuimarisha miundo msingi ya baadhi ya maeneo ambapo watalii wanapenda kuzuru ili kuwavutia zaidi.

Taarifa na Fatuma Rashid

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.