Idadi ndogo ya wanafunzi wajiunga na kidato cha kwanza Mombasa

January 11, 2018

KHALID- SHERIA-PIC

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limeelezea kughadhabishwa na idadi ndogo ya wanafunzi wanojiunga na kidato cha kwanza kaunti ya Mombasa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khalid amesema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi walioitwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za kaunti hiyo bado hawajaripoti shule.

Khalid anasema kuwa hali hii imesababisha Ukanda wa pwani kwa ujumla kusalia nyuma katika masuala ya elimu kutokana na wazazi kukosa kulipa kipaumbele suala la elimu.

Mkurugenzi huyo wa Haki Afrika amewahimiza wazazi na jamii ya ukanda wa Pwani kukumbatia vyema swala la elimu ili kuwawezesha watoto kupata haki zao za masomo sawia na kuinua viwango vya elimu katika kaunti za Pwani.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.