IDADI YA WATALII WA KIGENI YAONGEZEKA

November 7, 2018

 

Waziri wa utalii nchini Najib Balala amesema kuwa wizara ya utalii nchini imerekodi idadi ya watalii wa kigeni elfu 55 waliozuru humu nchini kuanzia mwaka 2016.

Akiongea alipowapokea watalii zaidi ya 120 kutoka nchini Uholanzi,  Balala amesema kuwa ongezeko hili la watalii linatokana na kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kutoka baadhi ya mataifa ya kigeni hadi jijini Mombasa mwaka wa 2016.

Faida iliyoandikishwa katika kipindi hiki imetajwa kufikia kima cha shilingi bilioni 3.7.

Balala amefichua kuwa mwaka huu wamepokea zaidi ya ndege 15 za watalii kutoka nchi za kigeni ikilinganishwa na mwaka jana ambapo walipokea ndege 9 pekee katika kipindi sawia.

Taarifa na Hussein Mdune.

 

 

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.