Idadi ya watoto wanaotungwa mimba yaongezeka Kinango

June 5, 2018

KAMISHANA WA KAUNTI YA KWALE KARUKU NGUMO

Idadi ya watoto wa kike wanaoacha shule na kukosa kuendelea na masomo katika gatuzi dogo la Kinango imetajwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Akithibitisha hilo Kamishna wa Kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema kuwa utafiti wa idara ya usalama kaunti ya Kwale umebaini kuwa chanzo kikuu ni wazazi kukosa kuwajibikia majukumu yao hali inayopelekea watoto wa kike  kuzurura ovyo na kuhudhuria sherehe za usiku na baadaye kupachikwa uja uzito.

Ngumo amewataka wadau mbalimbali kulitilia maanani suala hilo na kulizungumzia katika mikutano mbalimbali ili kutafuta suluhu la kudumu.

Aidha amewataka wazazi kukaza kamba katika ulezi wa wanao na kuwapa muongozo ufaao ili kukomesha tabia yao kuhudhuria ngoma za usiku.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.