Idara ya usalama kuangamiza magenge ya wahalifu Ng’ombeni

January 11, 2018

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imewaomba wakaazi wa eneo la Ng’ombeni gatuzi dogo la Matuga kushirikiana na idara hiyo ili kusaidia kuyaangamiza makundi ya kihalifu yanayowahangaisha wakaazi wa eneo hilo.

Kwenye mahojiano na mwanahabari wetu afisini mwake, Naibu kamishna  wa kaunti ya Kwale eneo la Matuga Benson Maisori amesema kwamba  vijana wanaoaminiwa kuwa  wanachama wa makundi ya kihalifu ya Wakali kwanza na Wakali wao yaliokuwa yakiwahangaisha wakaazi Mombasa sasa yametorokea  eneo la Ng’ombeni  wanapoendeleza uhalifu.

Maisori  amedokeza kwamba  tayari  maafisa wa usalama  wametoa ripoti  kuhusu  utovu wa usalama unaosababishwa na vijana hao wanaovamia na kupora watu mali zao.

Afisa huyo tawala  amesema kuwa  maafisa wa kitengo cha kukabiliana na ghasia kwa ushirikiano na maafisa wa upelelezi  , wameanza oparesheni katika eneo hilo ili kuhakikisha wahalifu hao wamekamatwa.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.