Idara ya usalama kuhusisha kitengo cha upepelezi katika kukabilianana wanafunzi watundu

July 10, 2018

Karuku Ngumo Kwale County commissioner

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeahidi kukihusisha kitengo cha upelelezi katika kukabiliana na masuala ya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi ikiwemo uharibifu wa mali ya shule.

Akizungumza na Mwanahabari wetu, Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema kitengo hicho kitatumika katika kufuatilia utovu wa nidhamu unayotekelezwa na wanafunzi shuleni.

Ngumo amedokeza kuwa upelelezi huo wa utovu wa nidhamu dhidi ya wanafunzi na matukio yake yatatumwa kwa serikali ili kutumika hata wakati wa maisha yao ya baadaye wanapotafuta kazi.

Ngumo ametaja kuwa wiki hii wakuu wa idara ya usalama pamoja na wadau wa elimu watatembelea shule kadhaa na kuongea na wanafunzi kuhusiana na madhara ya uchomaji wa shule miongoni mwa visa vyengine.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.