Ilianza na Dogo Richie, Lavalava na sasa ni Masauti

October 18, 2018

MSWAZI 29 06 17

Wakati Lava L ava alipoachilia kibao kwa jina Go Gaga wengi walisema kuwa aliiba wazo kutoka kwa msanii Dogo Richie aliyetangulia kuachia wimbo kwa jina hilo. Kabla vumbi halijatulia katika jambo hilo, msanii Masauti amezuka na kuja na kibao kinachoendana na maudhui hayo hayo.

Kupitia kursa zake katika mitandao ya kijamii Masauti ameachia kionjo cha Nyimbo itakayojulikana kwa jina Gaga.

“Je mpo tayari? Kibao Gaga nitakiwachilia hivi karibuni,” ameandika msanii huyo.

Ujio wake mpya umepokelewa vyema huku wasanii kama vile Nyota Ndogo akiisifia sana kwenye mtandao wa kijamii.

Swali hata hivyo linasalia kuwa pale pale, hivi iweje wasanii hawa wamekuja na nyimbo zilizo na maudhui sawa?

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.