Ingwe yabanduliwa na Singida

June 5, 2018

Timu ya mbili za Tanzania Simba na Singida zimefuzu kwa nusu fainali ya sportpesa Supa Cup.

Singida wamewabandua AFC Leopards kwa mikwaju ya penati 4-2. Katika muda wa kawaida timu hizo mbili zilitoka sare tasa.

Walioifungia AFC ni Robinzon Kamura na Whyvonne Isuza. Waliokosa ni Beka Dukoya, Mburu aliyepiga nje.

Katika muda wa kawaida Whyvonne Isuza alikosa mkwaju wa penanti.

Singida watachuana na Gor Mahia huku Simba wakipambana na Kakamega Homeboyz siku ya Alhamisi.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.