Jamii ya Wamakonde yahofia kufurushwa

January 12, 2018

Mwenyekiti  wa jamii ya Wamakonde  wanaoishi katika eneo la Msambweni kaunti ya Kwale Thomas Nguli, ameihimiza  serikali kuu na ile ya kaunti ya Kwale kuwatengea  watu wa jamii hiyo ardhi kuanzisha makao yao ya kudumu.

Akiongea na mwanhabari wetu, Nguli amedai kuwa wanatishiwa kufurushwa kutoka kwa makao yao ya sasa, jambo analosema limezua wasiwasi miongoni mwao.

Hata hivyo ameipongeza serikali kwa kuwasaidia wanajii hiyo kupata vitambulisho vya taifa, akisema kuwa   kwa sasa wanafikia huduma muhimu kutoka kwa serikali.

Aidha ameyaomba mashirika ya kijamii kuwashika mkono na kuwasaidia kupata haki zao hasa katika ugavi wa raslimali.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.