Jamii yahimizwa kukabiliana na mimba za mapema

January 13, 2018

Mwenyekiti wa muungano wa kitamaduni wa MADCA huko Malindi kaunti ya Kilifi Emmanuel Munyaya amewataka wazazi wa eneo hilo kuchukua jukumu la kuwalinda watoto wao ili kupunguza  ongezeko la mimba na ndoa za mapema.

Akiongea na mwanahabari wetu Munyanya amesema kuwa hatua ya wazazi kutowajibikia majukumu yao ya ulezi imechangia pakuzwa watoto hasa wa shule kupotoka kimaadili na kujiingiza kwenye anasa.

Munyanya aidha amesema watoto wa kike wako katika hatari zaidi kwani wengi wao hushindwa kuendelea na masomo yao punde wanapotungwa uja uzito.

Mwenyekiti huyo aidha amesema kuwa hatua hiyo pia huwa inachangia pakubwa ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa vijana na wakaazi wa eneo hilo kwa jumla.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.