Joho apata pigo mahakamani

January 11, 2018

Mahakama kuu mjini Mombasa imekataa ombi lililowasilishwa na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho la kumtaka aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar Sarai kufika Mahakamani.

Joho alikuwa anamtaka Sarai afike Mahakamani ili ahojiwe kuhusu swala lake la kumtaka Jaji Lydai Achode anayesikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Gavana Joho kujiondoa kwenye kesi hiyo.

Kupitia Wakili wa Joho, Mohamed Balala, aliyewasilisha ombi hilo mbele ya Jaji Lydia Achode amemtaka Sarai kuweka bayana kuhusiana na ombi lake la kumtaka Jaji anayesikiliza kesi ya Joho ajiondoe.

Hata hivyo Jaji Achode amepuuzilia mbali ombi hilo, akisema kuwa halina msingi wowote bali ni la kuonyesheana ubabe wa kisiasa.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.