Joho atembelea familia zilizoathirika na mafuriko Kadzandani

May 12, 2018

Gavana  wa Kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amesema kwamba imekuwa changamoto kwa Serikali ya Kaunti hiyo kuwazuia wakaazi kujenga katika maeneo yaliyo hatari hasa pindi kunaponyesha.

Joho ameitaja hali inayowakumba wakaazi wa eneo la Kadzandani eneo bunge la Nyali kama tata kwani zaidi ya familia 50 zimewachwa bila makao kufikia sasa baada ya nyumba zao kufunikwa na maji kutokana na mvua kubwa.

Akizungumza baada ya kuzitembelea familia hizo, Joho amesema kwamba japo Kaunti hiyo imekuwa ikipanga mikakati ili kuzuia hali hiyo, wakaazi wengi hawana maeneo mbadala ya makaazi  na wanaishi katika hali ya umaskini.

Gavana huyo amewafadhii waathiriwa hao kwa magodoro, vyakula na mahitaji mengine msingi ya kibinadamu.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.