Jubilee yapinga kuapishwa kwa Raila Mombasa

January 12, 2018

Baadhi ya Viongozi wa chama cha Jubilee kaunti ya Mombasa wameyakosoa baadhi ya mataifa ya kigeni kwa kuingilia masuala ya uongozi nchini.

Akiongea mjini Mombasa mwenyekiti wa chama cha Jubilee kaunti Mombasa Matano Chengo amesema kuwa taifa hili linaongozwa na katiba na haifai kwa mataifa hayo kuingilia siasa za Kenya.

Chengo aidha ameshtumu vikali hatua ya kinara wa NASA Raila Odinga ya kutaka kuapisha kama Rais wa wananchi tarehe 30 mwezi Januari akisema italeta mgawanyiko wa kikabila nchini.

Amemtaka Raila kujishughulisha na maswala ya kuleta wakenya pamoja kwa ajili ya maendeleo.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.