Kaa la Moto amwokoa Master Kimbo

November 24, 2018

Juma Mohammed maarufu kama Kaa La Moto amekuwa mtu wa hivi punde kumsaidia msanii Mastar Kimbo kutoka Kilifi aliyeathirika na madawa ya kulevya.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Instagram Kaa La Moto amepachika ukanda wa video akiwa ameandamana na Kimbo wakielekea kituo cha dawa ya Methadone.

Kimbo anaonekana akichana mistari katika video hiyo inayo ashiria kuwa amekubali kuacha mihadarati. Ishara hizi zimethibitishwa na ujumbe ambao Kaa La Moto ameupachika pamoja na video hiyo.

“Naona sio njema kudiscuss zaidi. Ila ilinibidi kurudi zangu kutoka safari kumwaisha hospitali na kumuanzisha utumizi wa Methadone,” ulisema ujumbe wa Kaa La Moto.

Mastar Kimbo ni msanii aliyevuma na kibao English Gold lakini utumizi wa mihadarati umemfanya kufifia kimziki.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.