Kaloleni United watoa cheche za vitisho

December 13, 2017

Baada ya kuwatitiga Congo Boyz na kuwafanya kuandikisha kushindwa kwao kwa mara ya kwanza msimu huu katika ligi ya FKF tawi la Pwani kusini, mkufunzi wa Kaloleni United FC Andrew Mwamba Kitsao amewaonya wapinzani wake atakao kutokana nao katika ligi ndogo ya tawi hilo.

Kaloleni United walihakikisha Congo Boyz hawamalizi msimu bila kushindwa kwa kuandikisha ushindi wa 1-0 katika mechi iliyochezwa wikendi.

Akizungumza na kituo hiki Kitsao amesema kuwa ushindi huo haukuwa bahati na wapo tayari kuwathibitishia mahasimu wao kwenye ligi hiyo ndogo itakayo andaliwa Mwakani.

Kitsao ameitaka Congo Boyz Kusahau kuhusu kunyakua taji la ligi na kujishughulisha zaidi na Chapa Dimba kwani tayari mshindi amejulikana.

Mkufunzi huyo pia amesema kuwa wanalenga kupandishwa daraja msimu ujao.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.