Kanisa lawataka viongozi wapwani kuungana

May 12, 2018

Askofu wa kanisa la Ushindi Baptist Joseph Maisha amewataka viongozi wa kidini ukanda wa Pwani kuungana ili kuzisaidia familia zilizoathirika na mafuriko.

Akiongea na wanahabari huko Likoni Askofu Maisha amesema kuwa kwa sasa familia nyingi zimepoteza makao na hata wapendwa wao kutokana na mafuriko yanayoendeelea kushuhuiwa katika maeneo mbali mbali.

Maisha hata hivyo ameilaumu serikali ya kitaifa kwa madai kwamba imeshindwa kujiandaa ipasavyo kukabiliana na majanga humu nchini.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.