Kariobangi Sharks washinda taji la SportPesa Super Cup

January 27, 2019

Klabu ya Kariobangi Sahrks ndio bingwa wa mchuano wa kimataifa wa SportPesa Super Cup.

Sharks wamepata ubingwa huo kwa kuilza Bandari goli 1-0

Sharks wamepata goli lao kupitia Harrison Mwendwa katika kipindi cha pili.

Kwa ushindi huu wametia kibindoni kima cha milioni 3 pesa za humu nchini na watakipiga na timu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza Everton.

Nambari mbili Bandari wamepata kima cha milioni 1 pesa za humu nchini.

Klabu ya Simba imemaliza ya tatu kw akuishinda Mbao FC kwa michuti ya penanti 5-3.

Taarifa Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.