Karua aitaka serikali kuwa wazi kuhusu Sukari hatari

July 12, 2018

Kinara wa chama cha Narck Kenya nchini Martha karua ameitaka serikali kupitia kwa wizara husika kuweka wazi kuhusiana na swala la sukari gushi nchini inayodaiwa kuwa na madini ya zebaki ambayo ni hatari kwa binadamu.
 
Akihutubu kwenye kongamano la pili la mahasibu wa kike mjini Mombasa Karua amesema kwamba ni jambo la kutamausha kuona kuwa mawaziri wamekuwa wakitoa taarifa kinzani kuhusiana na sukari hiyo  hali ambayo imechangia wananchi wengi kusalia njia panda wasijue ukweli upo wapi.
 
Karua amesema kuwa nijukumu la serikali kubaini ukweli kuhusiana na sukari hiyo ili wananchi wasiitumie endapo itakuwa na athari zozote za kiafya.
 
Wakati uo huo kinara huyo wa chama cha Narc kenya ameikosoa hatua ya waziri wa afya Sicily kaiuki kulinyamazia swala hilo ilihali linaathari za kiafya.
Taarifa na Hussein Mdune.
RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.