Katoi wa Tabaka afunguka kuhusu uhusiano wake na Nazizi

January 9, 2018

Siku za hivi karibuni msanii Katoi Wa Tabaka anayefanya mziki wa kisasa wa kitamaduni wa jamii ya Wamijikenda ameonekana akiwa katika ukaribu na msanii Nazizi hali iliyozua tumbo joto miongoni mwa wengi huku ati ati zikizuka kuhusiana na wawili hao.

Katika tukio la hivi majuzi wawili hao walionekana wakipiga picha pamoja wakiwa katika kiwanja cha ndege cha Malindi ambapo walitumia ndege binafsi kusafiri hadi kisiwa cha Lamu. Kisiwa ambacho Nazizi amekifanya nyumbani.

Katika pite pite zetu tulimpata Katoi na kukaa naye mkao ambapo alitufichulia kuwa uhusiano kati yao sio uhusiano unaodhaniwa na wengi bali ni uhusiano wa kikazi.

“Mimi na Nazizi ni marafiki wa kitamb sana. Ukiangalia tarehe 2 tulikuwa na Wyre kabla zijaelekea Lamu ambapo nilifanya tamasha na Nazizi,” alisema Katoi.

Aidha aliongezea kuwa kupitia kwa Nazizi aliweza kukutana na Dj anayepanga maonyesho yake na mwaka huu huenda akajumuishwa katika tamasha pamoja na Nazizi.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.