Kaunti ya Kilifi kujenga hospitali ya magonjwa sugu

September 4, 2018

KINGI (2)

Serikali ya kaunti ya Kilifi inapanga kujenga hospitali maalum itakayotumika kutoa tiba ya magonjwa sugu ambayo mara nyingi huwa ghali kama vile saratani.

Naibu gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Saburi amesema serikali ya kaunti itahakikisha hospitali hiyo ina mitambo ya kuchunguza magonjwa sugu na kutoa tiba kwa wagonjwa.

Saburi amesema waathiriwa wengi wa maradhi ya saratani hugharamika kusafiri hadi jijini Nairobi na kwengineko nje ya nchi kutafuta tiba, baadhi wakifariki mwishowe.

Hospitali hiyo itawahudumia wakaazi wa Kilifi na kote pwani ili kuhakikisha wanapata tiba nafuu kwa urahisi.

Taarifa na Mercy Tumaini.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.