Kaunti ya Mombasa yanunua mashini za kupuliza dawa ya kuua mbu

January 8, 2018

Serikali ya kaunti ya Mombasa imezindua rasmi mashine tano za kupuliza kemikali za kuuwa Mbu kama njia moja wapo ya kukabiliana na mkurupuko wa maradhi ya Chikungunya yaliokithiri katika kaunti hiyo.

Akizungumza baada ya kuzindua mashine hizo, Gavana wa kaunti hiyo Ali Hassan Joho amesema kuwa mashini hizo zimeigharimu kaunti ya Mombasa takribani shilingi milioni 15 na zitafanya kazi katika magatuzi yote madogo sita ya kaunti hiyo.

Joho amehoji kuwa serikali ya kaunti hiyo itahakikisha inaangazia zaidi maeneo yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa na maambukizi hayo ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Chikungunya.

Uzinduzi wa mashine hizo unajiri baada ya zaidi ya visa 100 vya maradhi hayo kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Mombasa huku maeneo la Mvita na Changamwe yakitajwa kuathirika zaidi na maambukizi hayo.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.