Kaunti ya Mombasa yapiga marufuku uuzaji wa maji na chakula barabarani

November 23, 2017

Serikali ya kaunti ya Mombasa imepiga marufuku biashara ya uuzaji wa vyakula na maji barabarani kufuataia kushuhudiwa kwa mkurupuko wa maradhi ya kipindupindu.

Akitangaza marufuku hiyo mjini Mombasa, Waziri wa Afya katika serikali ya kaunti ya Mombasa Bi Hazel Koitaba amesema kuwa hatua hiyo ni kuhakikisha wakaazi wa kaunti ya Mombasa wanaimarika kiafaya.

Hazel amedokeza kuwa marufuku hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia siku ya Ijumaa ili kudhibiti biashara zisizozingatia afya ya wakaazi sawia na kukabiliana na mkurupuko wa kipindupindu.

Waziri huyo aidha amesema kuwa idadi ya watu wanaougua maradhi hayo imeongezeka hadi watu 25 huku akisema kuwa wagonjwa hao wanatoka kaunti tofauti za ukanda wa Pwani.

Hata hivyo sehemu za Jomvu na Changamwe katika kaunti ya Mombasa zimetajwa kuongoza kwa idadi kubwa ya watu wanaougua maradhi ya kipindupindu.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.