Kaunti ya Taita Taveta kujenga soko la kisasa

January 4, 2018

Wafanyibiashara katika kaunti ya Taita Taveta wmepata afueni baada ya serikali ya kaunti hiyo kuweka wazi kwamba inamipango ya kujenga soko kuu katika kaunti hiyo.

Gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja amesema kuwa soko hilo litawasaidia wafanyabiashara wa kaunti hiyo hasa wakulima kuuza bidhaa zao na kuongeza mapato.

Gavana Samboja vile vile amedokeza kuwa tayari wamepata ardhi ya kujenga soko hilo huku akidokeza kuwa wanashirikina na mataifa ya nje kufanikisha ujenzo huo.

Taarifa na Fatma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.