Kaunti zakusanya kiwango cha chini cha ushuru

May 30, 2018

MVURYA 15 02 18

Mwenyekiti wa Tume inayosimamia ugavi wa ushuru nchini CRA, Jane Kiringai amefichua kuwa kiwango cha ushuru kilichokusanywa katika kaunti tofauti hasa mwaka uliopita kilikuwa wa chini mno.

Jane amesema tume hiyo sasa inalenga kuhakikisha kaunti zote zinakumbatia teknolojia ya kisasa ya ukusanyaji ushuru maarufu, Revenue Automation ili kuongeza juhudi za ukusanyaji wa ushuru.

Akizungumza katika kikao cha kujadili mbinu za kuimarisha ukusanyaji wa ushuru nchini kilichowaleta pamoja wadau mbalimbali huko Msambweni kaunti ya Kwale, Jane amesema tayari kaunti 33 humu nchini zinatumia teknolojia hiyo huku kaunti zingine zikitarajiwa kufuata mkondo huo.

Kwa upande wake Gavana wa Kwale Salim Mvurya ameitaka idara ya mawasiliano nchini kushirikiana na serikali za kaunti ili kufanikisha utumiaji wa teknolojia katika ukusanyaji ushuru nchini.

Taarifa na Salim Mwakazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.