Kenya waiadhibu Ethiopia

October 14, 2018

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars imeandikisha ushindi  wa 3-0 dhidi ya Ethiopia kwenye mechi iliyochezwa mbele ya mashabiki elfu 50 katika uwanja wa MSC Kasarani, Nairobi.

Kenya imepata ushindi huo kupitia mbao ya wachezaji Michael Olunga na Victor Wanyama.

Olunga ameipa Harambee Stars bao la kwanza baada ya kuupapatia mpira uliokuwa karibu na Eric Johanna katika dakika ya 23 ya mchezo.

Dakika nne baadaye Johanne alipachika wavuni bao la pili na kumpelekea naibu Rais William Ruto aliyekuwa akifuatilia  mechi hiyo mbashara,  kuruka juu kwa furaha.

Katika kipindi cha pili nahodha Victor Wanyama amefunga bao la tatu kupitia mkwaju wa penanti katika dakika ya 67.

Kwa ushindi huu Kenya imefuzu kwa AFCON mwaka 2019 iwapo FIFA itaendeleza marufuku iliyopiga Sierra Leone. Iwapo marufuku hiyo itaondolewa basi itahitaji pointi tatu zaidi ili kufuzu. Kwa sasa ipo na pointi saba.

Kenya inakutana na Ghana kwenye mechi ijayo ya kufuzu kwa AFCON, iwapo itafuzu hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2004.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.