Kesi ya kupinga ushindi wa Mwakilishi wadi ya Kakuyuni yatupiliwa mbali

November 30, 2017

Mahakama ya mjini Malindi imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na mpiga kura Athman Salim kupinga ushindi wa Mwakilishi wadi (MCA) wa Kakuyuni, Nickson Mramba kwenye uchaguzi wa Agosti 8.

Katika uamuzi huo uliotolewa na Hakimu mkuu wa mahakama hiyo Julie Oseko, mlalalamishi huyo ameshindwa kuthibitisha kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na dosari.

Hakimu Oseko amemuagiza mlalamishi huyo kulipa kima cha shilingi milioni 1.5 kama gharama za kesi hiyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wadi ya Kakuyuni kwa sasa Nickson Mramba ameupongeza uamuzi huo huku akisema kuwa yuko tayari kufanya kazi na wapinzani wake kuimarisha uchumi wa wadi hiyo. Kwenye uchaguzi wa Agosti 8 Mramba alipata jumla ya kura 3, 221 huku mpinzani wake akipata kura 1, 821.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.