Bodi ya filamu nchini imepiga marufuku uchezaji wa nyimbo za matusi hapa pwani hasa katika mazingira yalio na watoto wenye umri mdogo.
Afisa mkuu wa bodi hio kanda ya pwani Boniventure Kioko amesema kuwa Baadhi ya nyimbo zinazochezwa katika maeneo ya umma zimesheheni matusi hali inayowafanya watoto kupotoka kimaadili.
Kioko vile vile amesema kuwa maafisa wa bodi hio wataendeleza operesheni kali kwenye magari ya uchukuzi wa umma kuhusiana na suala hilo ,akisema kuwa watakaopatikana wakicheza nyimbo zisizokua na maadili wataadhibiwa.
Taarifa na Hussein Mdune.