Kingstone FC waibuka mabingwa

December 31, 2018

Prof Halimu Shauri akiwatuza Kingstone FC. Picha/ Ras Mangale

Prof Halimu Shauri akiwatuza Kingstone FC. Picha/ Ras Mangale

Klabu ya Kingstone FC ndio mabingwa wa makala ya kwanza ya “Unique Talents Mashinani”.

Kingstone wameibuka na ushindi kwa kuilaza Bongwe United kupitia mikwaju ya matuta baada ya kutoka sara ya bao 3 kwa 3 kwenye muda wa kawaida wa mchezo.  Mechi hio ilichezwa katika uga wa shule ya msingi ya Shamu Katika wadi ya Bongwe-Gombato.

Shirika la kijamii la HUDA ilikiongozwa na mkurugenzi wake Hon.Omar Boga ndio walioa andaa michuano hio iliyojumusha timu 32 huku 16 zikiwa za vijana wasiozidi umri wa miaka 16 ilhali zilizosalia ni kwa wale wasiozidi umri wa miaka 35.

Taarifa na Radio Kaya.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.