Klabu ya Bandari Youth yapongezwa

November 28, 2017

Mwenyekiti wa tawi dogo la FKF mjini Mombasa, Ali Goshi amevipongeza vilabu vilivyoshiriki katika ligi za tawi hilo mwaka 2017.

Kupitia kwa taarifa kwa vyombo vya habari mwenyekiti huyo amesema kuwa kushiriki kwa vilabu hivyo kwenye ligi ndiko kuliko fanikisha shughuli za soka za tawi hilo.

Goshi ameipongeza klabu vya Bandari Youth kwa kunyakua ushindi wa ligi ya Premia ya Mombasa na kutia moyo vilabu vingine kufanya vyema msimu ujao.

Goshi aidha ameahidi kuwa ligi zijazo zitakuwa na mabadiliko yatakayozifanya kuwa na ushindani zaidi.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.