Kosa analojutia Mzee Ngala

May 5, 2018

MZEE NGALA

Kwa miaka mingi Mzee Ngala amesifika kwa ufanisi wake katika mziki.

Yeye ndiye mwanzilishi wamziki wa Bango. Jambo ambalo limempa heshima miongoni mwa wasanii ukanda wa Afrika Masharika. Licha ya ufanisi huu ni jambo gani analojutia kufikia sasa?

Katika mazungumzo ya kipekee na mtangazaji wa kipindi cha Misakato Ya Bango Dominick Mwambui, Mzee Ngala amefichua kuwa kukosa kwenda Ulaya kwa ajili ya masomo ya mziki ndio jambo analojutia zaidi.

Kulingana naye alipata fursa ya kwenda ng’ambo kusoma lakini hakuweza kusafiri kwani alikuwa amefunga ndoa mwezi mmoja uliopita wakati huo.

Aidha amewausia wasanii wanaoibukia kuwa makini na kusomea taaluma zao ili kupata ujuzi zaidi.

Taarifa na Jumwa Mwandoro.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.