Kujumuishwa kwa watumizi wa mihadarati na familia zao kwapiga jeki vita dhidi ya mihadarati

May 5, 2018

Afisa wa miradi katika Shirika la ‘Reachout Centre Trust’ Mohamed Swaleh amesema kuwa kuwajumuisha watu wa familia katika harakati za kuwabadilisha tabia watumizi wa mihadarati kumeleta natija katika vita dhidi ya utumizi wa mihadarati hapa pwani.

Akiongea mjini Mombasa Swaleh amesema  juhudi hizo zimewawezesha wadau wa familia kuwaelewa watumizi wa dawa za kulevya.

Swaleh amesema wana familia wanatambua bayana kilichomsukuma mraibu kuingia katika utumizi huo na iwapo watashirikishwa katika harakati hizo watasaidia kumnusuru mraibu.

Kulingana na Swaleh, Shirika hilo linaandaa vikao kila siku ya Jumapili katika vituo vyake vya kuwarekebisha waraibu wa dawa za kulevya katika juhudi za kuihamasisha jamii kuhusu masaibu ya mraibu wa dawa za kulevya na jinsi jamii inavyoweza kuchangia katika kumnasua.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.