Kwale kupata shilingi bilioni 7.61 katika mgao wa fedha

January 8, 2018

SALIM MVURYA

Kaunti ya Kwale inatarajia kupata mgao wa kima cha shilingi bilioni 7.61 kutoka kwa serikali kuu katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Afisa anayehusika na masuala ya hazina kaunti ya Kwale Rama Kalama amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kuimarisha maendeelo ya kaunti hiyo.

Akiongea katika hafla ya kuchukua maoni ya wananchi kuhusiana na masuala ya bajeti iliofanyika katika ukumbi wa kitamaduni mjini Kwale, Kalama amesema kuwa kaunti ya Kwale inatarajia pia kukusanya shilingi milioni 600.

Kalama ametaja kuwa serikali ya kaunti ya Kwale pia inatarajia kukusanya kima cha shilingi milioni 288.75 kutoka kwa ushuru utokanao na raslimali zinazopatikana katika kaunti hiyo. Aidha ametaja kuwa katika bajeti yote shilingi bilioni 4.06 zitatumika katika masuala ya kimaendeleo huku bilioni 4.23 zikisimamia maswala ya ulipaji wafanyikazi

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.