Kwale kupokea vitabu elfu 30

January 10, 2018

Kaunti ya Kwale itapokea takriban vitabu elfu 30 vya kusoma kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwenye mpango wa Serikali wa kugawa vitabu katika shule za upili za umma.

Mwenyekiti wa Shirika la uchapishaji vitabu la ‘Kenya Literature Bureau’, Francis Baya, amesema kuwa vitabu vya somo la Kemia, Baiolojia na Kiingereza vitatolewa na shirika hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ugavi wa vitabu hivyo katika shule ya wasichana ya Matuga, Baya amesema kuwa vitabu vilivyosalia vitasambazwa na mashirika mengine yaliyopata zabuni hiyo.

Kwa upande wake Naibu Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Manza ameipongeza serikali kwa ufadhili huo, akisema kuwa vitabu hivyo vitawasaidia pakubwa wanafunzi wa shule hiyo ambao wengi wao wanatoka katika jamii zisizojiweza.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.