Lameck Boy apatwa na muujiza

May 3, 2018

Ikiwa unadhani kuwa miujiza haitendeki fikiria tena. Kwani iwapo mambo ya hivi majuzi ni ya kuzingatiwa basi miujiza bado ipo.

Msanii Lameck Boy ambaye ni producer wa Neptune records amewashangaza wengi baada ya kudai kuwa amepata miujiza wa uponyaji wa ugonjwa wa muda mrefu.

” Nimekuwa nikipitia mambo mengi sana yakifamilia na hata kwa kazi na afya yangu, lakini baada ya kuombewa nimepona kabisaa,” amesema Lameck Boy.

Kutokana na uponyaji huo ameamua kuachana na nyimbo za kidunia na kuimba injili.

“Huu ni uamuzi binafsi na namshukuru Mungu yeye ni Real Savior, ” amesisitiza msanii huyo.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.