Maambukizi ya virusi vya HIV yapungua Mombasa

June 29, 2018

Huku wizara ya afya kaunti ya Mombasa ikizindua rasmi zoezi la nyumba hadi nyumba la utafiti kubaini idadi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi, idadi ya watu wanaoishi na virusi hivyo katika kaunti ya Mombasa imepungua.

Kulingana na mkurugenzi wa afya kaunti ya Mombasa Dk Shem Patta  idadi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV imepungua kutoka asilimia 11.5 hadi asilimia 7.5.

Idadi kubwa ya wanaougua vizuri hivyo ni watoto.

Patta ameweka wazi kuwa utafiti huo ambao utachukua zaidi ya miezi sita kukamilika utasaidia kuimarisha viwango vya afya kwa wakaazi wa kaunti hiyo sawia na kufahamu asilimia kamili ya watu wanoishi na HIV.

Mkurugenzi huyo wa afya kaunti ya Mombasa amewahimiza wakaazi kutopuuza zoezi hilo.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.