Mabaharia mjini Mombasa wataka KMA kufanyiwa mabadiliko

January 24, 2019

Mabaharia mjini mombasa wamejitokeza na kuitaka   Serikali kufanya  mabadiliko ya uongozi  kwa mamlaka ya ubaharia nchini KMA  Kwa kile wanachodai kuwa imezembea kwenye majukumu yake ya kutatua changamoto zinazowakumba mabaharia.

Wakiongozwa na Hassan Kombo Ismail wamesema kuwa visa vya unyanyasaji kwa mabaharia wa Kenya vimekithiri mno kwani wamesema mabaharia humu nchini  hawathaminiwi kuliko wale wakigeni hatua anayoitaja kuvunja moyo za mabaharia.

Mabaharia hao aidha wameongezea kwamba  licha ya wao kupeleka malalamishi yao kwa mamlaka hiyo hakuna hatua zozote zinachuliwa na kupelekea wengi wao kuishi bila ajira.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.