Mabwenyenye waamurisha shule ya Mtomondoni kuvunjwa

July 10, 2018

Zaidi ya wakaazi elfu 50 wakiwemo wanafunzi elfu 5 wa shule ya msingi na ya upili ya Mtomondoni mjini Mtwapa kaunti ya Kilifi, wanaishi kwa hofu baada ya mabwenyeye kujitokeza na wakata kuondoka kwenye ardhi yao ya ekari 108.

Mabwenyenye hao wapatao kumi wanadaiwa kutoa ilani ya hadi mwezi wa nane kwa wakaazi hao kuondoka kwenye ardhi hiyo la sivyo watabomoa shule hizo pamoja na nyumba zao.

Wakiongozwa na Adam Athumani, wakaazi hao amedai kuwa hawataondoka kwenye ardhi hiyo huku wakiwataka viongozi wao kuingilia kati swala hilo na hata kuwapa hati miliki za ardhi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wadi wa eneo hilo Sammy Ndago amewahakikishia wakaazi hao kuwa swala hilo litasuluhishwa huku akimtaka Waziri wa ardhi na yule wa elimu kujadiliana jinsi watakavyokomboa ardhi hiyo. Wakati uo huo Mwakilishi huyo wa Wadi amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya ardhi Mohammed Swazuri kuzuru mashinani na kulitatua suala hilo.

Taarifa na Marieta Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.