Madaktari na wauguzi wafisadi kukiona cha mtema kuni Kilifi

July 12, 2018

ANISA OMAR 03 05 18

Wizara ya Afya katika kaunti ya Kilifi imewaonya kuwachukulia hatua kali za kisheria wauguzi na madaktari wanaojihusisha na ufisadi.

Akizungumza katika eneo la Langobaya eneo bunge la Malindi, baada ya kufungua rasmi zahati ya Sosobora, waziri wa Afya kaunti Kilifi Dkt Anisa Omar amesema kuwa wauguzi na madaktari watakaowatoza wakaazi ada kupata Huduma mashinani watakabiliwa kwani huduma zote za matibabu mashinani hazipaswi kutozwa ada yoyote.

Waziri huyo amekiri kuwa visa vya wagonjwa kuhangaishwa kuhusiana na malipo ya matibabu vimekithiri mashinani, wagonjwa wengi wakikosa kutafuta Huduma za matibabu kwa kukosa pesa ambazo hazipaswi kutozwa.

Bi. Anisa amehimiza ushirikiano wa wadau mbali mbali wa afya  na serikali ya kaunti ili kuimarisha huduma za matibabu katika kaunti ya Kilifi.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.