Madereva wahimizwa kujisajili

June 25, 2018

Madereva wa tuktuk katika kaunti ya Mombasa wamezidi kushinikizwa kujisajili kidigitali ili kuepuka visa vya uhalifu.

Akiongea mjini Mombasa mwenyekiti wa chama cha wahudumu wa tuktuk mjini Mombasa Obedi Muruli amesema kuwa kufikia sasa ni wahudumu 2,000 pekee waliosajiliwa.

Obedi amehoji kuwa kujisajili kidigitali kutawasaidia wahudumu hao kutambuliwa kwa urahisi wanapokumbana na visa vya utovu wa usalama barabarani.

Mwenyekiti huyo wa chama cha wahudumu wa tuktuk kaunti ya Mombasa amewahimiza wahudumu hao kuwa makini barabarani na kuripoti visa vya uhalifu wanavyokumbana navyo kwa chama hicho ili kushughulikiwa.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.