Maelfu ya pesa yachangishwa katika matembezi ya elimu Kwale

December 2, 2017

Shirika linaloshughulikia masuala ya elimu ya mtoto wa kike KWEA, limefanikiwa kuchangisha shilingi laki 3 na elfu 65 zitakazotumika kuwalipia karo wanafunzi kutoka familia zisizojiweza.

Shirika hilo limefanikiwa kuchangisha kiasi hicho cha pesa katika matembezi ya kilomita 10 yaliyofanyika  Msambweni kaunti ya Kwale.

Kulingana na Mwenyekiti wa shirika hilo, Mwaswere Juma kufikia sasa jamii haijazingatia elimu ya mtoto wa kike na matembezi hayo husaidia pakubwa kuinua viwango vya elimu.

Kauli yake imeungwa mkono na waziri wa fedha kaunti ya Kwale Bakari Sebe ambaye amewataka watoto wa kike kutumia muda wao vyema shuleni badala ya kujihusisha na mambo yasiyofaa.

Taarifa na Mwanakombo Juma.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.