Magoha aapa kukabiliana na waizi wa mtihani

October 30, 2018

Mwenyekiti wa Baraza kuu la mitihani nchini KNEC George Magoha amesisitiza  kuwa atahakikisha  mitihani yote ya kitaifa inayoendelea kote nchini inafanyika  bila ya udanganyifu wowote.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kasha la mitihani katika afisi za mshirikishi mkuu wa utawala Pwani mjioni Mombasa, Magoha amesema kuwa wameweka mikakati thabiti ya kuzuia udanganyifu wakati wa mtihani huo.
 
Magoha aidha amesema kuwa wanashirikiana na maafisa wa usalama kudhibiti visa vyovyote vya udanganyifu akitoa onyo kali kwa wenye nia ya kufanya udanganyifu.
 
Kwa upande wake Mshirikishi wa Utawala eneo  la Pwani, Bernard Leparmarai amesema kuwa karatasi za mtihani zimefika sehemu zote za ukanda wa Pwani ikiwemo maeneo ya Kiunga na Kiwayuu kaunti ya Lamu licha ya maeneo  hayo kuhofiwa kukabiliwa na changamoto za kiusalama.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.
RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.