Magunia 200 ya makaa yateketezwa Kilifi

June 8, 2018

Idara ya misitu  imeapa kuendeleza operesheni dhidi ya biashara ya uchomaji makaa sawa na ukataji miti katika msitu wa Dakacha kaunti ya Kilifi.

Akiongea katika eneo la Kamale baada ya kuteketeza takriban magunia 200 ya makaa, afisa mkuu wa idara hiyo kanda ya Pwani, Simon Wahome amewaonya wanaoendeleza biashara hiyo na kusema kwamba atakayepatikana atachukuliwa hatua kali za kisheria.

 Wahome aidha amehoji kwamba watahakikisha wanashirikiana na jamii ili kulinda msitu  wa Dakacha ili kukomesha ukataji wa miti ya kiasili ambayo imekua tegemeo katika maeneo kame.

Kwa upande wake afisa mkuu wa misitu eneo la Malindi, Harrison Afuata amesema kuwa eneo la Dakacha lina takriban ekari elfu 35 na huenda idadi ya maafisa walioko kwenye oparesheni hiyo wakashindwa kufikia maeneo mengine ambayo uharibifu wa misitu unaendelezwa.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.