Maji machafu yazorotesha biashara Kilifi

May 10, 2018

Wafanyibiashara katika Soko la OLoitiptip mjini Kilifi wamelalamikia kuzorota kwa biashara kutokana na maji chafu yaliyojaa na kuziba milango ya biashara zao.

Wakiongozwa na Boniface Odhiambo wafanyibiashara hao wamesema kuwa kukosekana kwa mitaro ya maji taka katika eneo hill ndio chanzo cha kurundikana kwa maji hayo yaliyochanganyika na takataka hali ambayo imekuwa vigumu kwa wateja kufikia biashara zao.

Kwa sasa wafanyibiashara hao wanahofu ya mpurupuko wa maradhi kutokana na maji hayo ambayo yamekaa kwa muda tangu mvua ianze kunyesha.

Aidha wameitaka serikali ya kaunti kuwajibika ili kutatua tatizo hilo.

Taarifa na Marrieta Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.