Makundi ya maendeleo kunufaika na milioni 6 Mombasa

May 17, 2018

Mwakilishi wa kike kaunti ya mombasa Bi Asha Hussein amesema kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa itayanufaisha makundi ya akina mama na vijana katika kaunti hio kwa shilingi milioni 6 fedha za kuwajenga kiuwezo.

Akizungumza katika eneo la changamwe Bi Hussein amesema kuwa kila wadi katika Kaunti hiyo itapata jumla ya shilingi laki mbili ili kuwawezesha walengwa kuwekeza katika miradi ya kibiashara  na kuukabili umaskini.

Bi Hussein hata hivyo amewasihi akina mama, Vijana na watu wanaoishi na ulemavu kuliangazia mno swala la uwekazaji, miradi ya biashara na kubuni ajira iliwajiimarishe kiuchumi.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.