Mali ya thamani isiyojulikana yateketea Kwale

February 8, 2019

Mali ya thamani isiyo julikana imeteketea moto katika mtaa wa Maramuni mjini Kwale, baada ya moto unaodaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme kuteketeza nyumba hiyo.

Kulingana na walioshuhudia mkasa huo, moto huo umetokea katika nyumba moja, na kusambaa katika nyumba zengine, huku mali yote kwenye nyumba hizo saba zikitekea moto.

Phyllis Nyaga, ambaye ni Mwalimu wa shule ya msingi ya Mwambara ni kati ya wapangaji waliopoteza mali yao kwenye mkasa huo.

Kwa upande wake Robert Nyanje ambaye pia amepoteza vifaa vyake vyote vya nyumba, amewaomba wasamaria wema kujitokeza ili kuwasaidia waathiriwa wa mkasa huo. Hata hivyo waathiriwa hao hawajaeza kubaini chanzo kamili cha moto huo.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.