Mambo wanayosoma Wakenya mtandaoni

June 5, 2018

Google imeachilia orodha ya vitu vilivyotafutwa sana mtandaoni mwezi wa Mei.

Suala lilotafutwa na wakenya wengi ni kuhusu ndoa ya kifalme ya Mwanamfalme Harry na muigizaji Meghan Markle iliyofanyika tarehe 19 Mei 2018.Wakenya waliingia mtandoani kupata ufahamu kuhusu familia ya kifalme na ndoa hiyo.

Mwezi huo pia uliwaona wakenya wengi wakisakura kuhusu mchuano wa Klabu Bingwa Ulaya UEFA uliofanyika Mei 26 ambapo Real Madrid walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Liverpool.

Kitu cha tatu kilichosomwa sana mtandaoni ni mechi kati ya Gor Mahia na Hull City iliyochezwa Mei 13.

Swala la nne lilopata usomwaji mkubwa ni kumhusu mrithi wa aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ambaye ni Unai Emery.

Kitu cha tano ilikuwa ni kuhusu mkasa wa bwawa la Solai ambapo watu 47 walifariki. Mkasa huo ulijiri baada ya bwawa hilo kuvunja kingo zake na kupelekea lita milioni 20 za maji kufunika kijiji cha Solai.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.