Maofisaa wa polisi waombwa kutotumia nguvu kupita kiasi

February 10, 2019

Wanaharakati wa kaunti ya Mombasa wamevitaka vitengo vya usalama hapa Pwani kuzingatia sheria vinapotekeleza majukumu yake.

Wakiongozwa na Fredrick Ojira wanaharakati hao wamesema kuwa idadi kubwa ya maafisa wa usalama katika kaunti hiyo hutumia nguvu kupita kiasi wanapowakabili washukiwa wa uhalifu.

Ojira aidha amesema kuwa ukosefu wa ushirikiano kati ya maafisa wa usalama na wanajamii hususan vijana kumechangia vijana wengi kukosa muelekeo na kujihusisha na mambo yasiyofaa.

Ameyasema haya kwenye mkao wa kujadili maswala ya usalama na Haki za binadamu mjini Mombasa.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.